Rais William Ruto ametaka usawazishaji wa shughuli za kibiashara kati ya Kenya na Japani, ili kutumia kikalimifu fursa zilizopo baina ya nchi hizo mbili.
Ruto alisema haya jana Jumatano alipokutana na mwenyekiti na pia afisa mkuu mtendaji wa shirika la biashara za nje nchini Japan, Norihiko Ishiguro, pembezoni mwa kongamano la tisa la kimataifa la Tokyo kuhusu maendeleo ya bara la Afrika – TICAD 9 mjini Yokohama, Japani.
Alisema kuwa Japani huingiza bidhaa za kima cha shilingi bilioni 130 humu nchini wakati Kenya ikiuza bidhaa za shilingi bilioni 9 pekee nchini Japani kutokana na vikwazo vya kibiashara.
Rais alisema Kenya inatafuta fursa zaidi katika soko la Japani, ikiwemo kwa bidhaa za kilimo kama vile maparachichi, maua na chai.