Rais Ruto amteua Mwenyekiti na Makamishna wapya wa IEBC

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amechapisha kwenye gazeti rasmi la serikali, uteuzi wa Erastus Edung Ethekon kuwa Mwenyekti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.

Ethekon sasa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Wafula Chebukati ambaye muhula wake wa kuhudumu ulikamlika Januari 2023.

Kwenye chapisho hilo la Jumanne jioni, kiongozi wa taifa pia alichapisha majina ya Makamishna sita wa Tume hiyo baada ya kusailiwa na kuidhinishwa na Bunge la Taifa.

Aliwateua Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Francis Odhiambo Aduol na Fahima Araphat Abdallah kuwa wanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kwa kipindi cha muda wa miaka sita.

Tume ya IEBC haijakuwa na Makamishna kwa muda wa miaka miwili na nusu, kufuatia kukamilika kwa muda wa kuhudumu wa Makamishna wa awali, akiwemo  mwenyekiti.

Uteuzi huo sasa unatoa fursa kwa Tume hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kuandaa chaguzi ndogo na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2027.

Hata hivyo uteuzi huo unajiri huku Jaji wa Mahakama Kuu akitoa maagizo ya kusitishwa kuapishwa kwa Makamishna wa Tume hiyo.

Share This Article