Rais William Ruto amemteua John Cox Lorionokou kuwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa.
Ikiwa uteuzi huo utaidhinishwa na Bunge la Taifa, basi Lorionokou ataziba pengo lililoachwa na Anne Nderitu ambaye kwa sasa ni Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Miapaka, IEBC.
Ruto pia amemteua Agatha Wanjiku Wahome kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Kisiasa.
Wakati huohuo, Claris Awuor Onganga ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu, KNCHR.
Hii ni baada ya mwanazuoni Dkt. Duncan Ojwang kukataa wadhifa huo.
Rais Ruto alikuwa amemteua Dkt. Ojwang kuwa mwenyekiti mpya wa KNCHR.
Katika kukataa uteuzi huo, Dkt. Ojwang alisema hatua yake imetokana na ababu za kibinafsi na mgongano wa maslahi ingekuwa angehudumu kwenye wadhifa huo.
Kulingana na taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Nairobi Hussein Mohamed, majina ya walioteuliwa yamepekwa katika Bunge la Taifa ili kupigiwa msasa na kuidhinishwa kwa mujibu wa sheria.