Rais William Ruto anahudhuria sherehe za kitamaduni za jamii ya Maasai katika mbunga ya Wanyama ya Amboseli kaunti ya Kajiado.
Sherehe hizo za kila mwaka huandaliwa kwa pamoja na kaunti za Kajiado na Narok na zinalenga kuhimiza udumishaji wa tamaduni za Kimaasai na ukuzaji utalii na hudumu kwa wiki moja.
Makala ya mwaka huu yaliyoanza Jumatatu wiki hii yatakamilika rasmi kesho Jumapili.