Rais Ruto ahimiza EU kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya AU

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akutana na Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya António Costa.

Kenya na Umoja wa Ulaya (EU), zinaendelea kufurahia ushirikiano thabiti  wa miaka mingi na ambao uliimarishwa kwa kutiwa saini mkataba wa makubaliano ya kiuchumi, ulioanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka 2024.

Rais William Ruto amesema mkataba huo unatoa fursa kwa bidhaa za kilimo za Kenya kufikia soko la EU bila ushuru.

“Tunatoa wito wa kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya Umoja wa Afrika, AU ili uweze kutekeleza lengo lake,” alisema.

Rais Ruto.aliongeza kuwa tajiriba ya Ulaya na uwezo wake wa kiteknolojia, utaiwezesha AU kushughulikia changamoto zake.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo alipokutana na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya António Costa, pembezoni mwa kongamano la saba la Umoja wa Afrika na ule wa Ulaya pamoja na kikao cha pili cha kamati maalum ya kutathmini utenda kazi kuhusu mageuzi ya kitaasisi katika AU nchini Angola.

“Tulijadili kuhusu hali ilivyo nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na maafa, janga la kibinadamu, uharibifu wa mali ya umma na ya kibinafsi na miundombinu,” alisema Rais Ruto.

Share This Article