Rais Ruto aelekea Addis Ababa kuhudhuria kongamano la Umoja wa Mataifa

Akiwa Ethiopia, Rais pia atafanya mazungumzo na viongozi kadhaa kutoka ulimwenguni na washirika wa kimaendeleo pamoja na sekta ya kibinafsi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesafiri kuelekea mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria kongamano la pili la Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa chakula.

Ruto anatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo kuhusu hatua zilizowekwa na Kenya kuhakikisha usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu.

Akiwa Ethiopia, Rais pia atafanya mazungumzo na viongozi kadhaa kutoka ulimwenguni na washirika wa kimaendeleo pamoja na sekta ya kibinafsi.

Pembezoni mwa kongamano hilo, Rais anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahamoud Ali Yousouf.

Share This Article