Rais William Ruto ameondoka nchini Jumapili kwa ziara ya mataifa ya Uingereza na Uhispania akilenga kutanua ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na mataifa hayo ya Ulaya.
Ruto anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Sir Keir Starmer, ambapo atasaini ushirikiano mpya wa Kenya na Uingerza kati ya mwaka 2025 na 2030 katika biashara,teknolojia,mabadiliko ya tabianchi na usalama .
Aidha Rais atahutubia mdahalo wa afrika utakaoandaliwa na shirika la Invest Africa, akielezea kuhusu mikakati ya iliyowekwa na Kenya kupanua wigo wa kibiashara.
Kabla ya kuzuru London, Ruto ataanzia ziara yake mjini Seville,Uhispania, atakapohudhuria kongamano la nne la kimataifa la uekezaji.