Raila: Tunapaswa kuweka mbele udhabiti wa taifa letu

Tom Mathinji
1 Min Read
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ameaga dunia.

Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, ametoa wito kwa Wakenya kuweka mbele udhabiti wa taifa, huku akiwataka viongozi wa serikali kuhakikisha sera za serikali, mipango na maamuzi zinatimiza maslahi ya wakenya wote.

Akizungumza leo Ijumaa wakati wa mkutano wa tatu wa Baraza la Mawaziri na viongozi wa serikali, Raila aliwakumbusha wote kuwa hakuna ufanisi utapatikana bila udhabiti na umoja wa kitaifa.

“Nazungumza kama yule ambaye ametembea na taifa hili kwa muda mrefu na ambaye anawazia mema taifa hili. Ninaamini kuwa bila kujali kutokubaliana kwetu, maono na kuvunjika kwa moyo, lazima tuweke taifa letu mbele,” alisema Raila.

Huku akizungumzia mkataba kati ya chama cha  ODM na UDA, Raila alisema mkataba huo ambao ulisababisha kubuniwa kwa serikali jumuishi chini ya uongozi wa Rais William Ruto mwaka jana, ulilenga kuimarisha udhabiti wa taifa hili.

Akipigia debe umoja wa kitaifa, kiongozi huyo wa chama cha ODM, alidokeza kuwa taifa ambalo limegawanyika, haliwezi timiza mageuzi yoyote.

Alitoa changamoto kwa viongozi wa serikali kuhakikisha umma haunufaiki tu na mipango ya serikali, lakini pia unajumuishwa katika kubuni sera na utekelezwaji wake.

TAGGED:
Share This Article