Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, ametoa wito kwa serikali kushikilia haki ya kikatiba ya Wakenya kuandamana, iwapo maandamano hayo yanatekelezwa kwa kuzingatia sheria.
Kiongozi huyo wa chama cha ODM alidokeza kuwa sehemu ya 37 ya katiba inawapa wakenya haki ya kuandamana na kuwasilisha malalalmishi yao kwa serikali.
“Maandamano huandaliwa kote duniani,kama vile hivi majuzi nchini Ufaransa, Uingereza, Netherlands, India na hata Pakistan wakati Israel ilipoishambulia Iran,” alisema Raila.
“Maandamano hayo yaliandaliwa bila kuvuruga shughuli za kila siku na uharibifu wa mali,” aliongeza kiongozi huyo wa ODM.
Matamshi ya Raila yanajiri kabla ya kuandaliwa kwa maandamano siku ya Jumatano Juni 25,2025, kuwakumbuka vijana walioangamia na wale waliojeruhiwa wakati wa maandamano ya kizazi cha Gen Z mwaka jana, kulalamikia Mswada wa Fedha wa 2024/2025.