Raila ataka serikali ilipe ridhaa kwa waathiriwa wa maandamano ya Gen Z

Raila alisema haya siku ya Jumapili katika kaunti ya Homa Bay, kwenye sherehe za 62 za siku kuu ya Madaraka.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, ameitaka Serikali kuwalipa ridhaa familia za walioathiriwa na maandamano ya mwaka jana ya vijana maarufu kama Gen Z, na waathiriwa wa maandamano ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2022.

Raila amesema ni kupitia tu ridhaa ambapo msamaha na maridhiano ya kitaifa utaafikiwa.

Raila alisema haya siku ya Jumapili katika kaunti ya Homa Bay, kwenye sherehe za 62 za siku kuu ya Madaraka.

Alisema kuwa msahama alioomba Rais William Ruto, wakati wa maombi ya kitaifa utakamilika kwa serikali kulipa ridhaa kwa wale waliojeruhiwa na kwa wale waliofariki kutokana na maandamano hayo.

Sherehe hizo ziliongozwa na Rais William Ruto.

Share This Article