Raia wawili wa Burundi washtakiwa kwa ulanguzi wa pembe za ndovu

Tom Mathinji
1 Min Read
Raia wawili wa Burundi washtakiwa kwa ulanguzi wa pembe za ndovu.

Raia wawili wa Burundi wamefunguliwa mashtaka katika mahakama moja ya Mombasa, kwa kushiriki biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori.

Gakiza Sulemani na Nkunubumwe Celecius, walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkaazi David Odhiambo, na kushtakiwa kwa kumiliki pembe 27 za ndovu kinyume na sheria.

Pembe hizo zenye uzani wa kilo 62.85, ni za dhamani ya shilingi 12,570,000.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa, washukiwa hao walikamatwa Agosti  3, 2025, saa tisa alasiri katika eneo la Miritini kaunti ya Mombasa, baada ya maafisa wa huduma za wanyamapori nchini (KWS), kupokea habari za kijasusi.

Aidha washukiwa hao wawili walikanusha mashtaka dhidi yao, na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi Milioni nne kila mmoja huku wakitakiwa kusalimisha hati zao za kusafiri.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 20, 2025.

 

TAGGED:
Share This Article