Ni afueni kwa raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC wanaopania kuzuru nchini baada ya serikali kuondoa masharti ya viza ili kuzuru nchini kuanzia Septemba mosi mwaka 2023.
Kulingana na serikali, agizo hilo linatokana na DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC mwezi Mei mwaka jana ambapo kwa kawaida, raia wa mataifa hayo hawahitaji viza ili kutembea miongoni nchi saba za jumuiya ya EAC.
Kabla ya kujiunga na jumuiya hiyo, raia wote wa kutoka DRC wamekuwa wakihitajika kulipia viza ili kuingia nchini Kenya.