Raia nchini Burundi leo Jumatano, watapiga kura kwenye uchaguzi wa kwanza wa wabunge tangu mwaka 2020, wakati Rais Evariste Ndayishimiye alipochukuwa hatamu zao uongozi nchini humo.Raia hao watawachagua wabunge 123.
Wengi wa wabunge hao watachaguliwa moja kwa moja kupitia vyama vyao huku wengine wakichaguliwa kama wabunge maalum. Chama cha rais Ndayishimiye cha National Council for the Defence of Democracy–Forces for the Defence of Democracy (CNDD–FDD) kilipata ushindi wa viti vingine bungeni wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020.
Utawala wa rais Ndayishimiye umekuwa ukikumbwa na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na dhuluma dhidi ya wanahabari,wanaharakati pamoja na upinzani.
Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa karibu na raia wa nchi hiyo pamoja na jamii ya kimataifa na utadhihirisha iwapo maafisa wa nchi hiyo watazingatia maadili ya kidemokrasia au la.