Paris Saint-Germain, ndio mabingwa wa taji ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kuwanyofoa Inter Milan mabao 5-0, kwenye fainali iliyosakatwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani.
Achraf Hakimi alipachika bao la kwanza dakika ya 12 ,kabla ya Doue kutanua uongozi kwa goli la pili dakika ya 20.
Doue aliongeza la tatu dakika ya 60 ,kabla ya Khvicha Kvaratskhelia kupachika la nne, naye Senny Mayulu akaongeza la tano.
PSG ndiyo timu ya pili kutoka Ufaransa kupata kombe hilo la kifahari baada ya Olympique Marseille, mwaka 1993.
PSG walifunga msimu kwa mataji matatu, ikiwa ni pamoja na ligi na kombe la Ufaransa.