Mabingwa wa Ulaya Paris St. Germain, PSG kutoka Ufaransa, walikuwa na mtihani mboga jana usiku baada ya kuwagaragaza mabinwga mara 15 barani humo Real Madrid mabao 4-0, na kujikatia tiketi kwa fainali ya Klabu Bingwa Duniani.
Fabian Ruiz, alifungua karamu ya magoli kwa PSG kunako dakika ya 6 katika semi fainali hiyo iliyosakatwa kiwarani Metlife huko New Jersy, Marekani.
Ousmane Dembele alitanua uongozi kwa goli la pili dakika tatu baadaye, kabla ya Ruiz kuongeza la tatu dakika ya 24.
Licha ya kujaribu kwa mashambulizi makali na kumiliki mpira, Real walishindwa kupenya ngome ya PSG katika kipindi cha pili.
Badala yake, Goncalo Ramos, aligongomelea msumari wa mwisho kwenye dau lililokuwa likizama la Madrid kwa bao la dakika ya 87.
PSG watashikana mashati na Chelsea Jumapili hii kwenye fainali ya mashindano hayo.