Prof. Mohamed Yakub Janabi, aliyependekezwa na serikali ya Tanzania, amechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO, kanda ya Afrika.
Janabi amechaguliwa wakati wa kikao cha WHO kilichoandaliwa Jumapili mjini Geneva, Uswizi.
Hadi kuchaguliwa kwake Priofessa Janabi, amekuwa Mshauri wa Rais wa Tanzania ,Masuala ya Afya na tiba na pia Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili .
Prof. Janabi amehitimsha na kipaumbele cha saba kwa kubainisha kuwa ataimarisha uzalishaji wa bidhaa za afya zikiwemo dawa, vifaa na vifaatiba pamoja na chanjo ndani ya Bara la Afrika.
Uteuzi wa Professa Janabi utaidhinishwa na bodi kuu ya WHO itakayokutana kati ya Mei 28 na 29 mwaka huu.