Rais William Ruto leo Jumatano amekutana na viongozi wa shirikisho la soka nchini pamoja na wawekezaji wa kibinafsi wa sekta ya michezo katika Ikulu ya Nairobi, kuweka mikakati ya maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.
Wakati wa mkutano huo, walijadiliana kuhusu mchango wa sekta ya michezo kuinua viwango vya michezo nchini hususan Kenya inapojiandaa kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027 pamoja na majirani wake, Uganda na Tanzania.
Mataifa hayo matatu yaliyoandaa maajuzi fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN, yamefuzu kushiriki AFCON mwaka 2027.