Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imetangaza zawadi ya kitita cha shilingi Milioni moja kwa yeyote atakayetoa habari zitakazofanikisha kukamatwa kwa Collins Jumaisi Khalusha, ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya wanawake ambao miili yao iliopolewa katika eneo la utupaji taka mtaa wa Kware, Nairobi.
Jumaisi, awali alikuwa amekamatwa lakini akatoroka kutoka kwa korokoro za polisi mwezi Agosti mwaka 2024, kabla ya kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka ya mauaji.
“Iwapo unafahamu aliko toa habari hizo kwa DCI kupitia namba isiyotozwa malipo 0800 722 203, au namba ya Whatsapp 0709 570 000.
Vile vile wananchi walitakiwa kutoa habari kwa kituo cha polisi kilicho karibu au kupitia namba za dharura 911,999 au 112.
Jumaisi alitoroka katika korokoro za polisi kwa njia tatanishi, baada ya kutiwa mbaroni alipohusishwa na mauaji ya wanawake Jijini Nairobi.