Polisi wapokea bunduki iliyosalimishwa Laikipia

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wapokea bunduki iliyosalimishwa Laikipia.

Maafisa wa polisi kaunti ya Laikipia wamepokea bunduki iliyokuwa ikimilikiwa kwa njia haramu.

Bunduki hiyo aina ya AK-47, ilisalimishwa katika eneo la Louniek, kaunti ndogo ya Kirima, na inahifadhiwa katika kituo cha polisi cha Olmoran kusubiri hatua zaidi kuchukuliwa.

Kupitia ukurasa wa X, Huduma ya Taifa ya Polisi ilisema hatua hiyo inaashiria ufanisi wa mchakato unaoendelea unaoongozwa na serikali wa kutwaa silaha zinazimilikiwa kinyume na sheria.

“Hadi kufikia sasa jumla ya bunduki 10 zimesalimishwa kwa hiari katika kaunti ndogo ya Kirima,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi.

Bunduki hizo ni pamoja na aina ya AK-47, moja aina ya carbine na risasi 56.

“Huduma ya Taifa ya Polisi inapongeza ushirikiano wa viongozi wa jamii ambao mchango wao ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa eneo hilo,” iliongeza NPS.

TAGGED:
Share This Article