Polisi wapata vifaa vya kieletroniki vya wizi mtaani Kayole

 Washukiwa hao wametiwa mbaroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Dismas Otuke
0 Min Read

Polisi wamepata vifaa vya kielektroniki vilivyoibwa mtaani Mihango, kaunti ndogo ya Kayole kaunti ya Nairobi.

Maafisa wa Polisi kutoka kituo cha Embakasi waliopokea taarifa za kijasusi kutoka kwa raia walipata vifaa hivyo vya wizi, ikiwemo rununu ya iPhone 15, simu nyingine 321 za rununu, vipakatalishi saba, na vifaa vya muziki vya LG.

 

Washukiwa hao wametiwa mbaroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Share This Article