Polisi wamekanusha kuhusika kwa mauaji ya mshukiwa aliyefungiwa kwenye korokoro ya Central jijini Nairobi kwa kueneza habari za uongo.
Kwenye taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya umma katika huduma ya taifa ya Polisi, mshukiwa huyo kwa jina Albert Omondi Ojwang, alijigonga kichwa kwenye kuta za korokoro hiyo na kupata majeraha yaliyosababisha kifo chake.
Punde baada ya polisi kubaini kuwa mshukiwa huyo alikuwa amejeruhia vibaya, walijaribu kumkimbiza katika Hospitali ya Mbagathi, lakini akaripotiwa kufariki punde baada ya kuwasilishwa.
Aidha, wameongeza kuwa mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa maafisa wa polisi (IPOA), imeanzisha uchunguzi kuhusu kifo hicho.