Polisi waadhimisha siku ya kimataifa ya kuzuia kujitoa uhai

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya kitaifa ya polisi ilijumuika na wadau siku ya Jumatano katika chuo cha Cooperative katika kaunti ya Nairobi kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuzuia kujitoa uhai.

Kwenye hotuba ya Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja, iliyosomwa na Mkurugenzi wa ushauri nasaha Evelyn Mbugua, alitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na idara hiyo kupunguza visa vya kujitoa uhai katika idara hiyo kama vile kufungua vituo vya utoaji ushauri nasaha,kutoa huduma za kidini,kutoa maafisa wa kisaikolojia na ushiriakiano na mashirika ya kimataifa kama Africa International University na  DMF-Kenya.

Kanja alihimiza umuhimu wa wanaothiriwa na msongo wa mawazo na matatizo ya kiakili na kumaliza unyanyapaa kama baadhi ya mikakati ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Share This Article