Polisi kaunti ya Samburu wapata mifugo waliokuwa wameibwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wapata mifugo walioibwa Samburu.

Maafisa wa polisi kaunti ya Samburu wamewapata mifugo waliokuwa wameibwa na kuwaokoa wafugaji dhidi ya kupata hasara.

Baada ya kupokea habari kuhusu wizi wa mifugo, maafisa wa polisi waliojumuisha wale wa kitengo cha GSU na polisi wa akiba, walitekeleza operesheni na kuwaandama wezi hao waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK47.

“Baada ya makabiliano makali ya risasi, maafisa wa polisi waliwazidi nguvu majambazi hao na kupata mifugo wotw 59 waliokuwa wameibwa,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi kupitia ukurasa wa X.

Kulingana na Huduma hiyo ya Polisi, mifugo hao 59 walikuwa wameibwa kutoka mfugaji mmoja eneo la Nchalai, Angata Nanyuki

“Mifugo hao tayari wamerejeshwa kwa mwenyewe,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi, ikiongeza kuwa itaendelea kuhakikisha usalama kwa wote.

TAGGED:
Share This Article