Polisi bandia anaswa Kirinyaga akiwa na sare

Mshukiwa huyo amewekwa korokoroni akisubiri kufikishwa mahakamani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa ujasusi kutoka kutoka kituo cha kaunti ndogo ya Kirinyaga East, wamemnasa polisi mmoja bandia aliyekuwa na sare na magwanda rasmi.

Polisi waliopata taarifa za kijasusi kutoka kwa wananchi walimemkamata Newton Wachira Waweru,ambaye baada ya kuhojiwa aliwapeleka polisi hadi nyumbani kwake mtaani Makongeni.
mjini Thika.

Msako uliofanywa  ulipelekea kupatikana kwa sare mbili za polisi,suruali ndefu mbili za polisi viatu vya polisi,bunduki bandia miongoni mwa vifaa vingine vinavyotumiwa na maafisa wa polisi.

Mshukiwa huyo amewekwa korokoroni akisubiri kufikishwa mahakamani.

Aidha, Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini endapo polisi huyo bandia alikuwa amewahadaa raia kwa kiwango kipi na ikiwa amejihusisha na visa vya uhalifu.

Share This Article