Pigo kwa wakuu wa shule baada ya serikali kuhamisha vyeti vya KCSE hadi kaunti

Dismas Otuke
1 Min Read

Ni pigo kwa walimu wakuu wa shule za sekondari humu nchini baada ya serikali kusema kuwa vyeti vyote vya kidato cha nne, KCSE vitakuwa vikichukuliwa katika afisi za elimu.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba alitoa amri hiyo wiki hii akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu.

Alisema kuwa hatua hiyo itamaliza uhuni wa walimu wakuu wa kukaidi agizo la serikali la kuwapa wanafunzi vyeti  bila masharti.

Walimu wakuu wamekuwa wakiwanyima wanafunzi walio na malimbikizi ya karo vyeti vyao.

Licha ya serikali mapema mwaka huu kuamrisha kutolewa kwa vyeti vyote vya wanafunzi, baadhi ya walimu wakuu walikiuka.

Share This Article