Papa Mpya atakayeongoza Kanisa Katoliki duniani hatimaye amechaguliwa.
Hii ni baada ya moshi mweupe kuonekana katika kanisa la Sistine huko Vatican muda mfupi uliopita baada ya ngoja ngoja nyingi miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.
Mchakato wa kumchagua Papa Mpya ulianza jana Jumatano ila haukufanikiwa mara ya kwanza.
Umati mkubwa wa watu umekusanyika katika eneo la St. Peter’s Square wakisubiri kutambulishwa kwa Papa huyo.
Papa Mpya atawasilishwa kwa umati huo wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, jina lake bado halijulikani wala haifahamiki anatokea nchi gani.
Jumla ya Makadinali 133 walipiga kura kumchagua Papa Mpya.
Waumini wa Kanisa Katoliki wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuchaguliwa kwa mrithi wa Papa Francis aliyefariki siku chache zilizopita baada ya kuugua.
Wengi wao walikusanyika katika eneo la St. Peter’s Square kusherehekea taarifa za kuchaguliwa kwa Papa Mpya.
Tutakuletea maelezo ya kina juu ya kuchaguliwa kwa Papa Mpya baada ya taarifa zaidi kutolewa,