Papa Leo azuru msikiti Uturuki

Tom Mathinji
1 Min Read

Papa Leo amezuru msikiti wa The Blue Jijini  Istanbul uturuki siku ya Jumamosi, na kuvua viatu vyake kama ishara ya heshima lakini hakushiriki sala wakati wa ziara hiyo.

Hii ni ziara yake ya kwanza akiwa kiongozi wa kanisa katoliki,katika eneo la ibada ya dini ya kiislamu.

Msikiti huo wenye uwezo wa kuchukua waumini 10,000, ulionyeshwa kwake na imamu na mufti wa Istanbul.

Akiwa amevaa soksi nyeupe, Leo alitabasamu, kutaniana na muezzin mkuu wa msikiti huo, na kuonyeshwa muonekano wa msikiti huo kwa dakika 20.

Papa yupo katika ziara nchini Uturuki hadi Jumapili, huku pia akipanga kutembelea Lebanon.

Katika sherehe ya pamoja na viongozi wa kikristo, alikosoa vurugu zinazofanywa kwa jina la dini na kuhimiza umoja mkubwa zaidi wa wakristo.

TAGGED:
Share This Article