Wingá wa klabu ya Paris St Germain Ousmane Dembele, ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ulimwenguni maarufu kama Ballon D’or kwa mara ya kwanza.
Dembele aliye na umri wa miaka 28 alimshinda nyota wa Barcelona na Uhipania Lamine Yamal.
Mfaransa huyo alikuwa nguzo muhimu kwa PSG kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza msimu jana walipoititiga Inter Milan mabao 5-0 kwenye fainali.
Kiungo wa Barcelona na Uhispania Aitana Bonmati alinyakua tuzo ya wanawake kwa mwaka wa tatu mtawalia.