Omanyala alemewa nusu fainali ya mita 100

Omanyala ambaye alimaliza katika nafasi ya saba mwaka 2023 mjini Budapest, Hungary ameambulia nafasi ya tano kwa muda wa sekunde 10.09.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya bingwa wa Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala kufuzu kwa fainali ya mashindano ya Riadha Duniani kwa mara ya pili mtawalia, imekatizwa leo baada ya kumaliza wa tano katika mchujo wa pili wa nusu fainali mjini Tokyo, Japani.

Omanyala ambaye alimaliza katika nafasi ya saba mwaka 2023 mjini Budapest, Hungary ameambulia nafasi ya tano kwa muda wa sekunde 10.09.

Fainali ya mita 100 itawashirikisha Wamarekani Kenneth Bednarek na bingwa mtetezi Noah Lyles, Kishane Thompson na Oblique Seville kutoka Jamaica, Letshile Tebogo wa Botswana, Kayinsola Ajayi wa Nigeria, Akani Simbine na Gift Leotlela wote kutoka Afrika Kusini na Zharnel Hughes wa Uingereza.

Share This Article