Mwanablogu Albert Ojwang’, anayedaiwa kuuawa na polisi yapata mwezi mmoja uliopita anatarajiwa kuzikwa leo kijijini Kokwanyo, kaunti ya Homa Bay.
Ojwanga ambaye pia alikuwa mwalimu wa sekondari, alifariki katika hali ya kutatanisha akiwa mikononi mwa polisi wa kituo cha Central kaunti ya Nairobi Juni 9.
Vurumai ilizuka jana baada ya waombolezaji kuvamia msafara uliokuwa na mwili wa marehemu na baadaye kuelekea hadi kituo cha Polisi cha Mawego na kukiteketeza .
Aidha, shughuli iliyopangwa ya kutazama mwili katika shule ya msingi ya Nyawango ilifutiliwa mbali.
Ojwang hata hivyo atazikwa kabla ya uchunguzi kumalizika kuhusu wote waliohusika kwa mauaji yake.
Marehemu aliyekuwa na umri miaka 31, alikamatwa na polisi Juni 7, akiwa nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa hadi Nairobi na kuripotiwa kufariki katika hali tatanishi siku mbili baadaye.