Ogallo atwaa dhahabu ya Taekwondo mashindano ya Africa Zone 5

Ogallo aliwazidia maarifa wachezaji wengine kutoka mataifa ya Uganda, Tanzania, Ethiopia, Rwanda, Djibouti, na Somalia.

Dismas Otuke
0 Min Read

Mchezaji Taekwondo wa Kenya Faith Ogallo, alinyakua nishani ya dhahabu ya uzani wa kilo 73 na zaidi katika mashindano wazi ya kanda ya tano Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kando na kubugia dhahabu Ogallo pia amefuzu kwa mashindano ya Afrika yatakayoandaliwa nchini Mali, baadaye mwaka huu.

Ogallo aliwazidia maarifa wachezaji wengine kutoka mataifa ya Uganda, Tanzania, Ethiopia, Rwanda, Djibouti, na Somalia.

Share This Article