Ofisi ya Umoja wa Mataifa yataka mauaji ya waandamanaji kuchunguzwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) imeelezea kusikitishwa wake kutokana na maandamano ya siku ya Saba Saba yaliyofanyika humu nchini jana Jumatatu.

Kwenye taarifa yake leo Jumanne, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk alisema inatia wasiwasi kwamba mauaji ya hivi karibuni yametokea siku chache baada ya waandamanaji wengine 15 kuuawa na wengine kujeruhiwa Juni 25.

“Ni muhimu kwa kiini cha maandamano haya kuangaziwa,” alisema Türk kwenye taarifa.

“Tuna fahamu kwamba polisi wamechunguza kuwa uchunguzi unafanywa juu ya visa vya awali. Kamishna Mkuu anasisitiza wito wake wa mauaji yote na madai ya ukiukaji mwingine na ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja utumiaji wa nguvu, kuchunguzwa kwa njia huru, ya wazi na madhubuti, ” aliongeza Türk kupitia msemaji wake Shamsani Rada.

Watu wasiopungua 10 wameripotiwa kuuawa wakati wa maandamano yaliyofanyika jana Jumatatu huku mamia wengine wakijeruhiwa.

Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS) inasema maafisa 52 wa polisi walijeruhiwa na watu 567 kukamatwa kufuatia maandamano hayo.

Share This Article