Nyumba yetu ilikuwa majaribio ya Vitendawili, asema Winnie Odinga

Dismas Otuke
1 Min Read

Kitinda mimba wa  marehemu Raila Odinga, Winnie Odinga, amewafurahisha waombolezaji waliofika katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, akimtaja babake kuwa alikuwa mwenye bashasha na busara tele.

Winnie ambaye ni Mbunge katika bunge la Afrika Mashariki (EALA) amesema vitendawili alivyokuwa akighani marehemu Raila katika mikutano ya kisiasa alikuwa akivifanyia majiribio akiwa nyumbani na wanawe.

Aidha amewapongeza Wakenya kwa kusimama na familia yao wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha babake.

Share This Article