Nyota wa Liverpool Diogo Jota afariki kwenye ajali siku 10 baada ya harusi

Akiwa Anfield Jota, alisakata jumla ya mechi 182 na Wekundu wa Anfiled akitikisa nyavu mara 65.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa klabu ya Liverpool Diogo Jota, amefariki mapema leo baada ya gari lake kuhusika kwenye ajali nchini Uhispania akiwa na umri wa miaka 28.

Mreno huyo aliyefunga pingu za maisha siku 10 zilizopita alikuwa na kakake mdogo Andre Silva, aliye na umri wa miaka 26, wakati gari hilo lilipopoteza mwelekeo na kushika moto katika mkoa wa Zamora nchini Uhispania.

Mshambulizi huyo alikuwa amefanya harusi na mchumba wake wa muda mrefu Rute Cardoso mjini Porto Ureno.

Akiwa Anfield Jota, alisakata jumla ya mechi 182 na Wekundu wa Anfiled akitikisa nyavu mara 65.

Mwendazake amemwacha mjane na watoto watatu.

Share This Article