Nyachae, Amadi miongoni mwa 37 waliorodheshwa kwa uenyekiti wa IEBC

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Msajili wa Idara ya Mahakama Anne Amadi na mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Utekelezaji Katiba (CIC) Charles Nyachae ni miongoni mwa watu 37 waliojumuishwa katika orodha ya wanaowania uenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC).

Wengine walio kwenye orodha hiyo ni pamoja na mwenyekiti wa bodi ya Kenya Power Joy Brenda Masinde-Mdivo, karani wa zamani wa bunge la kaunti ya Nairobi Jacob Ngwele, na wakili Duncan Ojwang.

Mwenyekiti wa jopokazi hilo, Dkt. Nelson Makanda, amesema wanawake sita na wanaume 31, wakiwemo watu watatu wenye ulemavu, ni miongoni mwa walio kwenye orodha hiyo.

Watu hao 37 waliteuliwa kutoka kwa orodha ya watu 1,319 waliosazwa baada ya mchujo wa kwanza.

Jopokazi hilo linatarajiwa kukamilisha kazi yake mwezi ujao ndani ya siku 90 ilizopewa kisheria, kabla ya kuwalisha majina kwa Rais William Ruto.

Mwenyekiti mpya wa IEBC atakayemrithi marehemu Wafula Chebukati, anatarajiwa kutangazwa mwezi ujao.

Share This Article