Mwenyekiti wa kamati ya afya katika Baraza la Magavana, Muthomi Njuki, anapendekeza msako mkali dhidi ya vituo vya afya vinavyotekeleza shughuli zao bila leseni akisema kuwa vinachangia kwa kiwango kikubwa vifo vinavyotokana na utepetevu.
Njuki, hata hivyo alisema kuwa kaunti zitashirikiana kwa karibu na wizara ya afya kuwaondoa madaktari wasihitimu wanaosimamia vituo vya afyakote nchini au wale wanaokodisha leseni zao kwa huduma katika sehemu tofauti nchini kwa kisingizio cha kunufaika kutokana na malipo ya serikali.
Njuki aliye pia Gavana wa Tharaka Nithi, alisema kuwa kamati hiyo imepokea ripoti nyingi kuhusu vituo vya afya vinavyotekeleza shughuli zao kinyume cha sheria huku vkihatarisha maisha ya wagonjwa kwa kutoahuduma duni.
Gavana Njuki, aliyasema hayo huko Mpukoni, kaunti ya Tharaka Nithi wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa kitengo cha matibabu ya kina mama chenye vitanda 40 katika kituo cha afya cha Mpukoni.
Aidha Njuki, aliunga mkono mpango wa SHA wa lipa na pole pole akisema ni nafuu ikilinganishwa na kulipa bili ya hospitali bila bima ya afya.