Katika kile kinachoonekana kama ulipizaji kisasi, Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby, siku ya Alhamisi alipiga marufuku utoaji Viza kwa raia wote wa Marekani siku moja baada ya Rais Donald Trump kutangaza kupiga marufuku utoaji Viza kwa raia wa Chad wanaotaka kuingia Marekani.
Trump alipiga marufuku utoaji viza kwa raia wa nchi 12 ikiwemo Chad, akitaja kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa.
Chad ndio taifa la kwanza kuchukua hatua hiyo, wakati ambapo Congo, ambayo pia iliwekewa vikwazo na Marekani, imejitetea ikisema kuwa ilitokana na kutoelewana.