Nimepoteza Rafiki Mkubwa ! Ezekiel Mutua aomboleza

Francis Ngala
1 Min Read
Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la Hakimiliki za Muziki nchini (MCSK) Dkt. Ezekiel Mutua anaomboleza kifo cha baba yake.
 
Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, Mutua alisema amempoteza rafiki mkubwa.
 
Mutua pia alipachika picha ya pamoja akiwa na Baba yake ambayo walipiga pamoja hapo awali akisema kuwa jioni kama hizo hazitakuwepo tena.
 
Aliongeza kuwa anashukuru kwa nyakati walizoshiriki pamoja na atahifadhi kumbukumbu hizo milele.
 
“Jioni kama hizi hazitakuwepo tena, lakini katika kila jambo, tunashukuru na kuthamini kumbukumbu hizo nzuri. Nimepoteza rafiki mkubwa. Nenda salama baba,” Mutua aliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Katika chapisho lingine, Dkt Ezekiel Mutua alisema ingawa si watu wengi wanaofikisha umri wa miaka 100, babake alifikisha umri huo na amefariki akiwa amezungukwa na vitukuu.

Aliongeza kuwa kifo cha baba yake kinamtia uchungu lakini ameacha urithi tajiri

Sio watu wengi wanaopata fursa ya kufikisha miaka 100 na kuondoka duniani wakiwa wamezungukwa na wajukuu na vitukuu. Baba aliona Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia na amepitia takriban njaa na magonjwa ya mlipuko katika historia iliyorekodiwa.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.