Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo amemtaja hayati marehemu Raila Odinga kuwa mwandani wa karibu na aliyeweka maslahi ya taifa mbele kwanza.
Obasanjo amesema haya Jumapili katika ibada ya mazishi ya Raila iliyoandaliwa katika chuo cha kiufundi na sayansi cha Jaramogi Oginga Odinga.
Aidha, Obasanjo amemtaja Raila kuwa kiongozi ambaye hakuwa na ubinafsi na mpiganiaji haki za wanyonge.