Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali ya Nigeria, kuwaondolea mashtaka watoto wanaozuiliwa kwa kushiriki maandamano kulalamikia gharama ya juu ya maisha.
Jumla ya watu 76, wakiwemo watoto 30 walifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa na kufunguliwa mashtaka 10, yakiwemo ya uharibifu wa mali, uhaini na kuvuruga amani.
Watoto hao wanadaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 14 na 17.
Picha za watoto hao wakizimia mahakamani, ziliibua hisia mseto kutoka mashirika ya kijamii na wanasiasa. Wamekuwa wakizuiliwa kwa muda wa miezi mitatu, tangu walipotiwa nguvuni mwezi Agosti mwaka huu.
Shirika la Amnesty International, lililaani kuzuiliwa kwa watoto hao, likitaja kuwa hatua za kuzima uhuru wa kukongamana.
Hata hivyo, Inspekta Jenerali wa polisi wa Nigeria, amepuuzilia mbali madai kwamba wafungwa hao wanateswa, akisema kuwa wote hao wamepokea huduma za matibabu.
Msemaji wa polisi Muyiwa Ogunjobi aliambia runinga moja ya Nigeria kuwa,” Mtu anapotimia umri wa miaka saba, unaweza fikishwa mahakamani,”.