Mabingwa mara tisa Nigeria almaarufu Super Falcons, ndio timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali ya kombe la Afrika kwa wanawake WAFCON, baada ya kusajili ushindi wa pili bao moja kwa bila dhidi ya Botswana jana kundini B.
Chinwendu Ihezuo alipachika bao pekee na la ushindi kwa Super Falcons, ukiwa ushindi wa pili baada ya kuilemea Tunisia mabao 3-0, katika mchuano wa ufunguzi.
Kwenye matokeo mengine Algeria na Tunisia waliambulia sare kappa.
Mechi mbili za kuhitimisha mzunguko wa pili hatua ya makundi zitapigwa leo, Mali ikipimana nguvu na Ghana kuanzia saa moja usiku katika kundi C, kabla ya Tanzania kukabana koo na mabingwa watetezi Afrika Kusini.