Nigeria kukwangurana na Chui Wa Congo fainali ya mchujo kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara nne wa Afrika Nigeria – Super Eagles – watachuana na the Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye fainali ya mchujo kufuzu kwa Kombe la Dunia Jumapili hii nchini Morocco.

Nigeria walijajaa fainali baada ya kuwankung’uta Gabon mabao 4-1, katika muda wa ziada baada ya sare ya bao moja katika muda wa dakika 90, katika uwanja wa Prince Moulay Hassan jijini Rabat.

Akor Adams alifungua ukurasa wa magoli akiwaweka Nigeria uongozini dakika ya 78, kabla ya Mario Lemina, kuwakomboa Panthers wa Gabon dakika ya 79 na kulazimu mechi kuingia dakika 30 za mazidadi.

Victor Osimhen atikisa nyavu Mara mbili huku Chidera Ejuke, akiongeza moja katika ushindi huo maridhawa.

DR Congo walihitaji bao la dakika ya 91 Lake Chancel Mbemba, kuwakwatua Simba Wa Cameroon goli moja katika nusu fainali ya pili ugani Elbarid jijini Rabat, na kuweka miadi ya kucheza fainali dhidi ya Nigeria.

Mshindi wa mechi hiyo ya Jumapili atacheza mchujo wa mwezi Machi mwaka ujao na timu ya kutoka bara jingine ili kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Kipute cha Kombe la Dunia kitaandaliwa kati ya Juni na Julai mwaka ujao katika mataifa ya Marekani, Mexico na Kanada.

Share This Article