Nicolas Sarkozy kuanza kifungo jela Jumanne

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.

Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ataanza kutumikia kifungo chake cha miaka tano gerezani leo Jumanne, baada ya kupatikana na makosa ya kupokea fedha za kampein kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi.

Sarkozy, aliyeongoza Ufarasa kati ya mwaka 2007 na 2012, anakuwa Rais mstaafu wa kwanza wa taifa la bara Uropa kufungwa gerezani.

“Sina uwoga wowote kwenda gerezani. Nitakuwa na ujasiri hata katika milango ya gereza,” alisema Sarkozy.

Atakapokuwa kuzuizini, Sarkozy hatakubaliwa kuwa na rununu lakini atakuwa na fursa ya kutumia simu ya kiusalama ya gereza hilo na pia atakubaliwa kutembelewa mara mbili kwa wiki.

Gereza la La Santé ni maarufu sana katika historia yake ya miaka 158, kwa kuwa miongoni mwa wale wamezuiliwa humo ni pamoja na gaidi sugu Carlos the Jackal na mhalifu wa kivita Maurice Papon.

Mwana wa kiume wa Sarkozy Louis, anayewania kiti cha Meya wa Menton, amewahimiza wafuasi kujitokeza karibu na nyumba ya Sarkozy, kumshangilia anapopelekwa gerezani siku ya Jumanne.

Share This Article