Ni vuta ni kuvute Jumamosi, Absa Kip Keino Classic

Katika mita 100, wanaume Ferdinand Omanyala, ambaye ni bingwa wa jumuiya ya madola, atamenyana na chipukizi wa Afrika Kusini Bayanda Walaza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Matayarisho yote yamekamilika kwa makala ya sita ya mbio za Kip Keino Classic continental Tour, zitakazoandaliwa  Jumamosi Mei 31, katika uwanja wa Ulizni Sports Complex, huku wanariadha wapatao 189 wakishiriki.

Bingwa wa Dunia wa urushaji sagai Julius Yego, atajitosa uwanjani dhidi ya bingwa mara mbili wa dunia Anderson Peters kutoka Grenada, ambaye pia alinyakua nishani ya shaba ya Olimpiki mwaka jana.

Katika mita 100, wanaume Ferdinand Omanyala, ambaye ni bingwa wa jumuiya ya madola, atamenyana na chipukizi wa Afrika Kusini Bayanda Walaza.

Mita 800 wanawake zitamshirikisha bingwa wa dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, Saarah Moraa, dhidi ya Lillian Odira na Maloney Shafiqua kutoka kisiwa cha Saint Vincent, walioshiriki Olimpiki mwaka jana.

Mashindano hayo ya siku moja yatashirikisha vitengo vitatu vya kitaifa na vya hiari kabla ya kukamilika kwa kitengo cha kikuu kuanzia saa kumi na dakika 29 kwa mbio za mita 800 wanawake .

Share This Article