Timu ya taifa Harambee Stars itamenyana na Angola leo Alhamisi katika mchuano wa pili wa kundi A, kuwania kombe la CHAN.
Mechi hiyo itasakatwa katika uwanja wa Kasarani kuanzia saa moja usiku.
Makocha wa timu zote wanalenga ushindi ili kuafikia azima zao mbalimbali.
Kocha wa Kenya Benni McCarthy alisema jana Jumatano kwamba wako tayari kuikabili Angola ingawa ni mpinzani mgumu, lengo kuu likiwa ushindi.
Naye mwenzake wa Angola Pedro Gonsalves, alisema amesoma mchezo wa Kenya na wanalenga kushambulia tokea mwanzo ili kupata ushindi.
Angola ilipoteza mechi ya kwanza mabao 2-0 dhidi ya Morocco, nayo Kenya ikailaza DR Congo goli moja kwa nunge.