Ni siku ya ndovu kumla mwanawe CHAN ikianza leo kwa Mkapa

Kenya,Uganda na Tanzania zinaandaa kipute hicho kwa pamoja kuanzia leo hadi Agosti 30.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye makala ya nane ya fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani CHAN yatangóa nanga leo.

Mchuano wa ufunguzi utasakatwa kuanzia saa mbili usiku leo katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam, Tanzania, huku wenyeji wakipimana ubabe na Burkina Faso katika kundi B.

Kabla ya fainali hiyo kutakuwa na sherehe za ufunguzi kuanzia saa moja usiku.

Kenya,Uganda na Tanzania zinaandaa kipute hicho kwa pamoja kuanzia leo hadi Agosti 30.

Viwanja vitano vya Benjamin Mkapa jijini Dar, Mandela mjini Kampala, Uganda, Kasarani na Nyayo jijini Nairobi, na Amaan nchini Zanzibar vitaandaa kwa pamoja mechi 44 za CHAN.

Mataifa hayo yanatumia CHAN kujipima kuandaa kindumbwendubwe cha AFCON mwaka 2027.

Kenya itaandaa mechi 13 zikiwemo 7 uwanjani Kasarani zikijumuisha mechi za kundi A za Harambee Stars na robo fainali.

Share This Article