Ni kufa kupona kwa Angola wakikabana koo na Zambia, CHAN

Angola watayaaga mashindano wakikosa kupata ushindi huku Zambia wakiwa bado na fursa ya kufuzu kwa robo fainali hata wakipata sare.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Angola almaarufu the Palancas Negras, itachuana na Chipolopolo kutoka Zambia leo katika mchuano wa kuwania kombe la CHAN uwanjani Nyayo.

Pambano hilo litaanza saa kumi na mbili jioni, timu zote zikiwinda ushindi wa kwanza, baada ya Angola kupigwa na Morocco na kwenda sare na Kenya huku Zambia wakicheza mechi ya pili baada ya kushindwa na DRC kwa mabao 2-0.

Angola watayaaga mashindano wakikosa kupata ushindi huku Zambia wakiwa bado na fursa ya kufuzu kwa robo fainali hata wakipata sare.

Share This Article