Mwanamuziki wa Marekani Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo amesimulia kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi ambayo yanajumuisha wanawake wengi.
Akizungumza katika mahojiano, Ne-Yo alisema kwamba yeye huwa hafichi lolote kutoka kwa wale ambao anahusiana nao, wakiwemo wanawe.
Mwimbaji huyo alisema kwamba kila anapokutana na mrembo anayemfurahisha, huwa anamwambia ukweli kwamba ana wapenzi wengine na iwapo hana tatizo na hilo anamkaribisha kwenye orodha ya wapenzi wake.
Ne-Yo ana watoto wawili na Monyetta Shaw-Carter, watatu na Crystal Renay na wawili na Sade Jenea na alisema kila anapoulizwa na wanawe yeye huwajibu kikweli kwamba wanawake wote ni wapenzi wake.
Mfumo huo wa wapenzi wengi hata hivyo uliwahi kumkwaza Shaw-Carter, ambaye aliwahi kukiri kwenye mahojiano kwamba uhusiano wao uliharibika pale ambapo walikaribisha mwanamke mwingine.
Hata hivyo Ne-Yo anasema kwamba awali alijisumbua sana kimawazo wakati alikuwa akijihusisha na wanawake wengine kisiri na mpangilio wake wa sasa unamridhisha kwani hadanganyi yeyote.
Haya yanajiri wakati ambapo mwanamuziki huyo anadaiwa kuongeza mwanamke wa nne kwenye mahusiano yake ya kimapenzi.