Mwanamuziki nyota wa muziki wa Rap nchini Afrika Kusini Nasty C anapeleka ziara yake ya kikazi almaarufu Ivyson Tour jijini Kampala nchini Uganda.
Jina Ivyson limetokana na jina la marehemu mamake mzazi aliyeitwa ‘Ivy’ na ziara hiyo ya kikazi ni ya kumkumbuka.
Tamasha la Uganda litaandaliwa kesho Novemba 7, 2025 huko Motiv katika eneo la Bugolobi na litafikia kilele kwa awamu ya pili ya kongamano la Aumex.
Tukio hilo la hadhi ya juu linaandaliwa na Talent Africa Group kwa ushirikiano na Aumex, na linaungwa mkono na wadhamini wakiwemo Guinness Toorly, NRG Radio, na SafeBoda.
Nasty C atakuwa jukwaani na wasanii kashaa wa Uganda kama Echoled, City Girl, Expect Xhavi, Son of Aboda, Vini Mercy, Tungi, na DJ Tony.
Tamasha hili litakuwa la kipekee likutoa burudani nzuri kwa mashabiki huku likiangazia msanii wa kimataifa pamoja na kina cha muziki wa kikanda.
Kongamano la Aumex, ambalo ni mkutano mkuu wa biashara ya muziki nchini Uganda, litafanyika kuanzia tarehe 6 hadi 8 Novemba.
Lengo kuu la mkutano huo ni kuwawezesha wasanii wa Uganda, watayarishaji, na wataalamu wa tasnia ya muziki kwa kuwapa fursa ya kufikia masoko na nafasi za kimataifa.
Ratiba ya siku tatu itajumuisha vipindi vya mafunzo ya kitaaluma, vipindi vya kujenga mahusiano na maonyesho ya muziki.