Nasty Blaq amtaka Peller arejelee masomo

Blaq anahisi kwamba Peller angekuwa na tabia bora iwapo angepata masomo zaidi.

Marion Bosire
2 Min Read
Nasty Blaq

Mwigizaji na mchekeshaji wa Nigeria Nasty Blaq amezua mjadala mitandaoni baada ya kumtaka mshawishi maarufu wa TikTok Peller arejelee masomo.

Nasty alikuwa akizungumza na wafuasi wake mtandaoni ambapo alitoa maoni yake akisema kwamba wengi wanasema kwamba elimu ni kashfa tu na sio muhimu lakini tabia ya Peller imedhihirisha kinyume cha dhana hiyo.

“Maneno ambayo wengi wanasema sasa nchini Nigeria ni kwamba elimu ni kashfa tu lakini Peller amekosoa usemi huo kwa tabia yake” alisema Blaq akiongeza kwamba Peller anahitaji kurejea shuleni.

Alimtaka mshawishi huyo wa mitandaoni wa umri mdogo aweke kando hela nying alizonazo na arejelee masomo akimshauri kwamba sio lazima aende shuleni na sio lazima afike chuo kikuu bali anaweza kuajiri walimu wa kumfunza nyumbani.

Peller naye hakuchelea kujibu maoni ya Nasty Blaq ambapo alisema maoni hayo hayahitajiki bora wafuasi wake mitandaoni wanamuelewa.

“Maoni yako hayahitajiki bora watu wananielewa. Hawa waigizaji wote wa mitandaoni hawakwenda shule. Utawaona tu wakijipatia riziki.” alisema Peller.

wanamitandao nchini Nigeria wamegawanyika katika mvutano huu kati ya nyota hawa wawili. Wapo wanaomuunga mkono Nasty Blaq huku wengine wakimuunga mkono Peller.

Huku haya yakijiri, mhubiri mmoja kwa jina Kesiena amekashifu vitendo vya Peller na mpenzi wake Jarvis mitandaoni akilalamika kwamba wanapotosha vijana.

Kulingana naye, mambo mengine wanayofanya hayafai kwani hawajaoana.

Share This Article